Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

GEORGE TAYSON NAYE KATUTOKA KWA AJALI YA GARI

Msanii na muongozaji wa sinema tanzania GEORGE TAYSON amefariki dunia katika ajali yagari iliyotokea maeneo ya Gairo.
Habari za awali zinasema George tayson alikuwa na wenzake wakitokea dodoma kwenye moja ya kazi zake za udirector na ndipo wakakapata ajali maeneo yua gairo. walikuwa wamekwenda dodoma kwa ajili ya kipindi cha The mboni show.
kwa wale wasiomkumbuka vizuri George Tayson ni yule aliyeongoza filam ya Girlfreind aliyocheza TID enzi hizo, Tayson alikuwa mume wa msanii maarufu wa maigizo na filam maarufu kama MONALISA na walifanikiwa kupata mtoto mmoja.
Kabla ya kifo chake Tayson alikuwa anaongoza kipindi cha the Mboni show kinachorushwa na televisheni ya East Africa. mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya morogoro kwa ajili ya kusubiria taratibu nyingine.
Watu wengi wameshtushwa na kifo hiki hasa ukizingatia kuwa ni Juzi tu ametoka kuzikwa msanii mwingie  aitwaye Rachel.
mwezi huu ni kama ulikuwa na mkosi kwa wasanii wa tasnia ya sinema kwa ni ndani ya wiki mbili misiba minne. wiki mbili na vifo vinne vya wasanii, hii ni kali ya mwaka.
MoDesign tunawapa pole wafiwa wote, familia ya marehemu na dada yetu Monalisa. Pole sana mamy.
MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top