Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KHADIJA KOPA AFUNGUKA KUHUSU BIFU LA DIAMOND NA ALI KIBA

Khadija Kopa, ni mwanamuziki wa Taarab mwenye jina kubwa sanaa hapa nchini Tanzania na mbaye alikuwepo katika show moja iliyofanyika Dar na kukatokea tafrani za wasanii kurushiwa makopo wakiwa jukwaani.
Khadija Kopa amesema hakupendezwa na tukio hilo kwa kuwa inawavunja moyo wasanii wetu hao ambao ni wawakilishi wetu wa nchi.
KUHUSU BIFU LA DIAMOND NA KIBA

Malkia huyu wa Mipasho alizungumzia pia mastaa wawili wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Diamond na Ali Kiba akasema kama kuna hali ya kutokuwa na maelewano kati yao ni vizuri wakakaa na kumaliza tofauti zao kwa kuwa hata yeye na marehemu Nasma Khamis Kidogo walikuwa marafiki ila mashabiki ndio walikuwa wanarushiana vijembe kupitia nyimbo zao.
akasema kuwa mashabiki wamekuwa ni watu ambao wanatengeneza bifu zao huko mitaani kwao kulingana na mapenzi yao kwa wanamuziki hao, lakini kumbe huku waliko wanapatana na pengine hata kuchangiana mawazo ya kikazi. 
Una kila haki ya kupata kila Stori inayonifikia Beste wangu, endelea tu kufuatilia modesigntz
USISAHAU PIA KU LIKE PAGE YETUILI NAWE UWE MWANACHAMA NA HABARI ZETU ZIWE ZINAKUFIKIA MOJA KWA MOJA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top