Millard Ayo, ni jina ambalo sio geni masikioni mwa watu wengi sana Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla. huyu kwa sasa ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM na vilevile ni mmiliki wa Mtandao maarufu wa millardayo.com.
mimi nimemfahamu millard Ayo kama miaka minne iliopita, tulipokuwa tunafanya naye kazi ITV/R ONE. ni kijana ambaye alionekana kuwa mbunifu na mwenye mitazamo tofauti na mitazamo ya watu wengine mbao nilikuwa nimewazoea. na siku zote nilijua atakuwa na kitu special ambacho alikuwa nacho kichwani, na ndicho hiki nilichokishuhudia leo katika ukurasa wake wa Intagram.
Kaika ukurasa wake wa Instagram millard Ayo aliandika mneno haya.
"... siku zote ni furaha pale ndoto inapokuwa kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu, na leo namshukuru mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidisign hii na baadae watu wangu @francis_ayo na @abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani nina mengi ya kutaja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA!! Thanks kwa maboss wangu Joe Kusaga ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu!
Birthday yangu ilikuwa Jan 26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa.
posti hii ilifuatiwa na comment kibao zenye kutoa pongezi.
Hongera sana Mdogo wangu Millard Ayo.
Endelea kufuatilia modesigntz beste wangu, na mimi ntaendelea kukuwekea kila story inayonifikia.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILINA WEWE U WE MWANAFAMILIA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE MAOJA KWA MOJA.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN


Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.