NI ARUSHA
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Triple A, jijini Arusha ambapo mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006 alienda kwenye sherehe ya mmoja wa rafiki zake huku yeye akipewa ‘taito’ ya mgeni rasmi.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini kilidokeza kuwa hivi karibuni, Kiba alikuwa na shoo maalum mjini Arusha ambayo ilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji hilo ambapo siku hiyohiyo, Wema naye alikuwa na marafiki zake wakisherehekea na wenyeji wake, hivyo baada ya kuisha na kusikia Kiba yupo mjini hapo, akaona ni fursa nzuri ya kwenda kumuona.
“Wema alialikwa na rafiki yake mmoja hivi huku Arusha sasa baada ya sherehe yao kuisha na kuambiwa Kiba anaangusha shoo, akaona bora aibuke Triple A akamuone,” kilisema chanzo hicho.
TEAM KIBA WAMZUIA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, baadhi ya wapambe wa Kiba (Team Kiba) waliposhtukia mchezo huo, walimzuia Wema getini ili asiweze kuonana naye.
“Wema alikuja majira ya saa 7:45 usiku akiwa na timu yake, kufika pale walitaka kuingia, lakini kwa hali aliyokuwa nayo wakakataa kumruhusu. “Walijua lazima angefanya kitu kwa Kiba, kitendo ambacho wao hawakupenda, hivyo mabaunsa wakafanya kazi yao vizuri.
“Kitendo cha kumkatalia kuingia kilisababisha kizaazaa hasa kutoka kwa wapambe wake. Ilitokea patashika nguo kuchanika kabla ya kukubali yaishe na kuondoka zao,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuvutiwa waya na kusomewa mashtaka, Wema alitiririka; “Ni kweli nilikuwa Arusha kwa shughuli zangu, nilifikia Mount Meru ambayo pia baadaye Kiba naye alifikia na tulionana, usiku kulikuwa na pati ya marafiki zangu, tukawa huko tulipomaliza tukaenda kwenye shoo ya Kiba.
“Kwa kweli sikumbuki chochote maana siku hiyo nilikuwa nimelewa sana, kwa hiyo nashindwa kusema kama unachosema nilikifanya au la, ila kesho yake niliambiwa kuwa tulikwenda kwenye shoo ya Kiba na hatukuingia.
“Hata wakati wa kurudi hotelini kwetu sikujua nilifikaje, zaidi ya kesho yake asubuhi niliwasikia kina Martin wakisema kwamba tulienda Triple A lakini kweli hatukuingia kutokana na fujo zilizokuwa zimejitokeza pale hivyo tukaamua kurudi kulala.”
Endelea kufuatilia modesigntz, na mimi ntaendelea kukuwekea kila habari inayonifikia
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI NAWE UWE MWANAFAMILIA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE HAPO ULIPO.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN



Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.