Katika ‘iventi’ hiyo, Madam Rita alikuwa beneti na Zari hivyo baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi na kudhani labda Madam alikuwa kama bodigadi’ wa Zari ili kusaidia linapokuja suala la kumwaga ung’eng’e a.k.a kutema yai lakini imebainika kwamba wawili hao ni ndugu kabisa.
Ilifahamika kwamba, Zari amekuwa akikutana na Madam Rita mara kwa mara anapokuwa Bongo, ikiwa ni pamoja na kushauriana mambo kibao ya kimaendeleo hasa katika suala zima la kuona fursa kwenye ishu za burudani.
Kwa mujibu wa Madam Rita, mbali na undugu, anamkubali Zari katika pilikapilika za kusaka maisha lakini pia Zari naye anamkubali Madam Rita kwa harakati zake za utafutaji na kupambana na umaskini.
“Zari ni mwanamke mtafutaji na ni ndugu yangu kabisa. Unajua pale Mlimani City watu walikuwa wanauliza tupoje, wengine walidhani nipo na AKA (msanii wa Afrika Kusini) lakini ukweli ni kwamba mimi na Zari tunafahamiana vizuri,” alisema Madam Rita.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.