Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MAM'DO LISA SEHEMU YA 26... SHUKA NAYO...






ILIPOISHIA SEHEMU YA 25

Dennis alishituka na kuingiwa na uoga kuwa mama yake anaweza akamkuta baba yake na Msichana wa kazi chumbani kwao akawa anamuangalia mama yake kisha anaangalia mlangoni katika chumba cha wazazi wake kama watatokea....

SASA HII HAPA SEHEMU YA 26

.... Alipoingia chumbani kule Hasina alianza kutafuta hicho alichotumwa na bosi wake lakini alikuwa hajakiona, aliendelea kutafuta bila mafanikio, ni dhahiri kwamba Mzee Bisu alimtuma akachukue kitu ambacho hakipo, lakini akiwa anaendelea kutafuta ghafla alishituka kumuona mtu akisimama nyuma yake alipogeuka akakutana uso kwa uso na Mzee bisu, akataka kumwambia kuwa alichomtuma hajakiona lakini kabla hajafanya hivyo Mzee huyo alimrukia na kumkumbatia kisha akamwambia kwa sauti ya chini
“... nilitamani sana kuukumbatia mwili wako mpenzi wangu ndio maana nikakutuma huku...” aliongea hivyo akiwa amemkumbatia kisha akamuachia na kumtazama moja kwa moja machoni.
“... kwani wewe na Dennis mna agenda gani... mbona siwaelewi?..” aliuliza Mzee Bisu.
“... aka... kati yangu na Dennis hakuna chochote kinachoendelea...” alijibu Hasina kwa kuinua mabega juu
“... sasa mbona mko karibu na mnafuatanafuatana, kwani vipi...” aliendelea kuuliza mzee huyo akitaka kufahamu kama ni kweli mwanaye anataka kumuingilia kwenye anga zake au la. lakini kabla hajapata jibu kutoka kwa Hasina wote wawili walishitushwa na muungurumo wa gari likipaki, walibaki kimya kwa muda kisha Hasina akatamka na huku akijinasua kutoka mikononi mwa mzee huyo.
“... mkeo huyo karudi, niache mimi nitoke zangu...” aliongea kwa harakaharaka, lakinbi Mzee Bisu aliendelea kumshikilia
“... subiri Hasina,.. leo usiku usifunge mlango, nitakuja sawa?..” aliongea Mzee Bisu kisha akamuachia Hasina ambaye hakujibu kitu akaanza kutoka, aliuvuta mlango ambao ulikuwa umejirudisha na kutaka kutoka, lakini akasita na kurudi nyumba haraka. ni kwamba alipokuwa akitoka macho yake yalianza kutangulia kule anakoelekea, na hapo ndipo alipomuona Bi. Pauline akipita sebuleni pale kuelekea Jikoni akiwa na mifuko yake mikononi. mzee Bisu naye alishituka na kumuuliza kwa wahka.
“... vipi?..”
“... mkeo,.. amepita kuingia jikoni,,, ngoja niondoke...” alijibu kisha akachungulia tena, hakuona mtu zaidi ya kumuona Dennis akiwa anamkodolea macho. alitoka kwa mwendo wa haraka.
alipoingia jikoni Bi. Pauline aliweka mezani mizigo yake kisha akaanza kutoka tena kurudi sebuleni huku akiongea kwa sauti.
“.. Dennis, kwani huyu Hasina yuko wapi?..”
lakini swali hilo lilimkuta Hasina akiwa tayari amefika pale sebuleni na yeye ndio akalijibu swali badala ya Dennis.
“... niko hapa mama,.. za huko,..” alijibu na huku akitembea kuelekea hukohuko jikoni.
“... ulikuwa wapi mbona sijakuona nilivyoingia,.. alihoji Bi. Pauline.
Hasina aligeuka nyuma kumuangalia Dennis kIsha akageuka na kujibu swali lake kiupole.
“... nilikuwa huko nyuma nilikuwa namalizia kufanya usafi, niliposikia ukipaki gari ndo nikaja...” alijibu kwa kirefu na huku wakati mwingine akigeuka kumtazama Dennis kama ataongea chochote, lakini Dennis alikuwa kimya akiwatazama tu.
“... haya nenda jikoni uanze kuandaa chakula nilishakuletea kila kitu...” aliongea Bi. Pauline na huku akiondoka kuelekea chumbani kwake. Hasina naye aligeuka kwa mara ya mwisho kumtazama Dennis kisha akaondoka kuingia jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula.
kabla hajafika chumbani kwake Bi. Pauline alikutana na Mume wake naye akitoka, Mzee Bisu alikuwa na wasiwasi lakini alijaribu kuficha wasiwasi wake kwa kujifanya anamuuliza swali mke wake lisilo na msingi.
“... mbona umewahi kuirudi mama Dennis, umefika sokoni kweli?..” alihoji huku akipishana na mke wake. mkewe naye alimjibu huku akipita.
“... ndio, si nilikwenda na gari langu...” alijibu kisha akaingia chumbani, na kila mtu akaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Dennis alitaka kuanza kupata hisia kuwa baba yake atakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Hasina lakini alikuwa akijaribu kutafuta pointi ya msingi ya kulithibitisha hilo akaikosa, kwani kuingia chumbani kwa baba yake Hasina alitumwa na kwa vile hakukiona alichotumwa ndio baba yake akamfuata huko kwa hiyo hakuna pointi yakuthibitisha hisia zake hizo. akaamua kuendelea na mpango wake wa kumnasa Hasina, lakini ajabu kwa siku hiyo ilikuwa ngumu kupata hata dakika moja ya kuongea naye kwani kila alipotaka kuwa karibu na Hasina baba yake naye alikuwepo au mama yake. mpaka inafika wakati wa kwenda kulala hakupata nafasi hiyo. akajipa moyo kuwa kesho yake itakuwa ni siku ya jumapili nafasi itakuwa yake kwani wazazi wake wote watakwenda kanisani, hivyo akawa mvumilivu.
*************************
Hadi saa nane za usiku Mzee Bisu alikuwa hajapata hata lepe la usingizi, akili yake yote ilikuwa imehamia kwa Hasina, mwili ulikuwa umemsisimka vibaya na alikuwa anavutavuta muda ili mke wake alale fofofo ili yeye akajilie vyake chumbani kwa Hasina. na ndivyo ilivyo kuwa kwani mida hiyo Bi. Pauline alikuwa anakoroma kama pono. Mzee Bisu alimkagua mara mbilimbili kuhakikisha kuwa amelala kweli.
“... yes... alijisemea mwenye baada ya kugundua kuwa mkewe tayari kalala...” alijishika mdomo kujizuia kutamka neno lingine kwani hata lile yes, lilimtoka tu kulingana na furaha aliyokuwa nayo, alinyanyuka taratibu akavaa bukta lake nataulo akalitupia shingoni akaanza kunyata taratibu, akaufungua mlango wa chumbani kwake taratibu huku akigeuka kumuangalia mkewe japo chumbani kulikuwa na giza. alifanikiwa kuufungua kisha akachungulia sebuleni kwanza kabla hajatoka maana mwanaye Dennis huwa na kawai ya kuangalia tv hadi usiku wa manane. sebuleni kulikuwa shwari, akatembea kwa mwendo wa haraka kidogo, akapita sebuleni na kuusogelea mlango wa chumba cha Hasina, akaangalia huku na huku kuhakikisha kama yuko salama, na kweli hakuona mtu, akakishika kitasa cha mlango wa Hasina na kukizunguusha taratibu, kitasa kikakubali sheria na mlango ukafunguka akageuka tena nyuma kuhakikisha usalama wake Mara macho, yakamtoka pima kama mtu aliyeona jini....

ITAENDELEA... USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA 27

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top