Wanafunzi wanaodaiwa kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
KABANG! Staa
anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa
International jijini Dar ambao aliahidi kuwalipia ada,
Chanzo makini kililiambia gazeti hili
juzi kwamba, baada ya Diamond kuwashindanisha watoto hao, Hillary na
Hamis katika shindano la Ngololo lililonyika Januari, mwaka
jana katika Viwanja vya Leaders Club, Dar na kushinda aliamua kuwapeleka
katika shule hiyo na kuahidi kuwalipia ada kila mwaka lakini kuanzia
hapo aliwatelekeza.
“Jamani Diamond kila kukicha anafanya
shoo za mamilioni lakini ameshindwa kuwalipia ada wale watoto ambao
aliahidi kuwasomesha. Wamesoma mwaka mmoja tu, mwezi uliopita
walitimuliwa na sasa wako nyumbani. Inauma sana kwani hawa watoto
walitolewa kwenye shule za kawaida na yeye ndiyo akawapeleka kule,”
kilisema chanzo hicho.
WAZAZI WANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Fadhili alisema watoto wao walitimuliwa shuleni tangu April mwaka huu kwa kuwa, Diamond hakuwahi kuwalipia ada tangu alipowaingiza pale.“Inauma sana, kwani tangu watoto wetu watimuliwe tumekuwa tukifuatilia kwa mtu tuliyeambiwa ni msimamizi wa Diamond (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) lakini hatupi jibu la kueleweka.

Nasibu Abdul ‘Diamond akiwa na wanafunzi hao pamoja na mwalimu wao.
“Tulipewa namba za simu za mameneja wa
Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella lakini kila
tukiwapigia simu tunaambiwa msanii huyo hayupo Dar, mara amesafiri, mara
yuko kwenye shoo, yaani kila siku tunazunguka tu hatujui tufanye nini.
“Tunaomba sana jamani, mtusaidie na nyie
waandishi maana watoto wanapitwa na masomo na isitoshe kabla ya hapo
walikuwa wakisoma kwenye shule za kawaida,” alisema mzazi huyo.
MSIKIE MWALIMU MKUU
Paparazi wetu alifunga safari mpaka shuleni hapo maeneo ya Mikocheni, Dar na kufanikiwa kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Mercy Githirua ambapo alithibitisha watoto hao kusimamishwa masomo kutokana na kukosa ada.“Tulivumilia kwa muda mrefu sana kwani tulimwamini Diamond tukawapokea watoto hao na kuanza masomo. Siku aliyokuja kuwakabidhi hapa shuleni aliomba ‘invoice’ kwa ajili ya kututumia ada lakini yuko kimya mpaka leo.

...Akisalimiana na mwalimu.
“Hata fedha ya kuwashonea sare za shule
ilibidi niwasiliane na (linatajwa jina, linasitiriwa) maana tunafanya
naye kazi nyingi, akatoa hizo fedha lakini ada ndiyo ikawa tatizo. Hivyo
ilipofika Aprili 14, mwaka huu ilibidi niwarudishe nyumbani mpaka
kieleweke kwa kweli.
“Sijapenda tabia ya Diamond, hivi anajua
watoto wakimchukia itakuwa ni hatari sana kwake? Watoto wa watu
walikuwa wanasoma huko akaenda kuwatoa na kuwaleta hapa lakini
amewatelekeza, siyo vizuri kabisa,” alisema mwalimu mkuu huyo.
WANADAIWA SHILINGI NGAPI?
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, watoto hao tangu walivyoingia Januari 21, 2014 hawakuwahi kulipiwa ada yoyote hivyo kila mmoja anadaiwa shilingi milioni moja na laki sita (1,600,000).
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, watoto hao tangu walivyoingia Januari 21, 2014 hawakuwahi kulipiwa ada yoyote hivyo kila mmoja anadaiwa shilingi milioni moja na laki sita (1,600,000).
Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
DIAMOND, MAMENEJA WAKE!
Juzi, gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kwa njia ya simu lakini ilikuwa imesetiwa kwamba inafanya kazi muda wote ‘bize’ hata alipotumiwa meseji hakujibu. Vivyo hivyo kwa mameneja wake, Fella na Bab Tale simu zao ziliita bila kupokelewa.

TUJIKUMBUSHE
Mwaka jana, Diamond aliandaa shindano la Nani Anaweza Kucheza Staili ya Wimbo wa Ngololo ambapo watoto kibao walijitokeza Leaders Club. Watoto hao wawili waliibuka kidedea kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza na ndipo zawadi yao aliamua kuwapeleka kwenye shule hiyo na kukutwa na yaliyowakuta!

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.