Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

STEVE NYERERE UMEKUA...ACHANA NA MABIFU... SHUKA NAYOI...

KWAKO Steven Mengere‭ ‬‮!‬٪Steve Nyerere‮!&‬‭ ‬mambo vipi swahiba‭? ‬Bila shaka utakuwa uko poa na unaendelea na majukumu yako ya kila siku‭.‬
Ukitaka kujua afya yangu‭, ‬mimi ni mzima kabisa naendelea na mishemishe kama kawaida‭. ‬Nimekukumbuka leo kupitia barua maana kitambo kidogo hatujaonana‭, ‬si unajua tena majukumu‭!‬
Madhumuni ya barua hii kwanza ni kutaka kukukumbusha kwamba sasa hivi wewe jina na umri wako ni mkubwa katika sanaa ya filamu Bongo‭.‬
Nakukumbusha kwamba kutokana na heshima yako‭, ‬hupaswi kuwa na tofauti na wenzako tena ukizingatia nyinyi kama wasanii mnapaswa kuwa kitu kimoja ili muweze kuisogeza tasnia yenu mbele kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu‭.‬
Ndugu yangu Steve‭, ‬kwanza nikwambie tu kuwa natambua mchango wako katika masuala mbalimbali ya tasnia‭. ‬Wewe ndiye unayewaunganisha wenzako‭, ‬ndiye unayefanikisha masuala mengi ya Bongo Movies kwenda sawa‭.‬
Nimeshuhudia hilo katika raha na matatizo kama misiba na mambo mengine‭. ‬Umehamasisha michango na kweli mambo mengi yalifanikiwa‭ ‬kwa ajili yako‭.‬
Pamoja na hayo‭, ‬juzi nilisikia sakata lako kutuhumiwa na wenzako kuwa umechakachua fedha za kujengea kaburi la Adam Kuambiana‭. ‬Sitaki kuingia sana kwenye kiini cha sakata hilo lakini binafsi sikufurahishwa na malumbano yako na mwigizaji mwenzako Kulwa Kikumba‭ ‬‮!‬٪Dude‮!&‬‭ ‬na William Mtitu‭.‬
Hamkupaswa kulumbana‭. ‬Nyinyi wote ni wasanii‭. ‬Kama kuna tatizo mnapaswa kuelezana na kulimaliza‭. ‬Mabifu hayana maana yoyote‭.
‬Kwa‭ ‬nini mlumbane‭? ‬Kwa nini ufikie hatua ya kutoa maneno mazito kama yale mtandaoni kwa wenzako‭?‬
Hukuwa na haja ya kuanza kuwatuhumu kina Mtitu kama wamewalipa waandishi ili wakuchafue‭, ‬watawalipa shilingi ngapi‭? ‬Una uhakika‭ ‬gani‭? ‬Mbaya zaidi tukio hilo liliripotiwa na magazeti ya Global Publishers ambayo yanasimamia weledi‭, ‬usitegemee hata siku moja‭ ‬mwandishi anaweza kununuliwa na mtu ili akuchafue wewe‭.‬
Mlipaswa kusimama katika hoja ya msingi‭, ‬mkazungumza kiutu-uzima na mkaelewana‭. ‬Kuanza kuingia kwenye mitandao ya Instagram na kuporomosheana shutuma nzito hakuna maana yoyote‭.‬Muungwana hata kama utakuwa umemuudhi kiasi gani‭, ‬hutumia busara kumaliza jambo lake‭. ‬Nikushauri‭, ‬kaeni chini wewe pamoja na wenzako mmalize tofauti zenu kuliko kutafutana uchawi‭, ‬ili iweje‭? ‬Maisha yenyewe mafupi‭, ‬Mungu anatutaka tupendane‭.‬
Upendo ni nguzo kubwa sana ya maisha mazuri ya kumfurahisha Mungu‭. ‬Waite kina Dude na Mtitu‭, ‬kaeni chini mzungumze na mmalize hili suala‭. ‬Kumbukumbu inaonesha si mara moja umekuwa ukiwatuhumu wasanii hao kwamba hawakupendi‭, ‬wanatamani ufe kitu ambacho si kizuri‭.‬
Kama kuna sehemu wewe ulikosea‭, ‬usiwe mzito kuomba msamaha na kama wao kuna mahali walikosea‭, ‬wakuombe radhi na kuanzia hapo mfungue ukurasa mpya wa maisha na mkuze soko lenu la filamu‭.‬
Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa‭, ‬niwatakie maisha mazuri ya upendo‭! ‬Bwana awe nanyi‭!‬
Ni mimi swahiba wako‭,‬
‭...................‬
Erick Evarist‭.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top