Mke wa Edward Lowassa, Regina Lowassa akikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Hakuna ubishi kuwa jina la
Edward Lowassa limepamba vichwa vya habari nchini kwa miezi kadhaa huku
gumzo jipya kumhusu mwanasiasa huyo likitokana na safari yake ya
kuelekea muungano wa nyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kutangazwa.
Lowassa alitajwa juzi jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alipozungumza na
waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya chama mshirika wa muungano huo
cha Wananchi (Cuf) kwa lengo la kukaribishwa.
Baada ya taarifa hiyo kuenea kwenye
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mjadala mpya ulizuka miongoni
mwa wananchi kwa kila mmoja kujaribu kuelezea hatima ya mwanasiasa huyo
maarufu nchini.
“Walimwaga mboga, kamwaga ugali, mwaka
huu kitaeleweka, CCM kimeuza silaha,” John Peter aliandika ujumbe huu
katika akaunti yake ya Twitter.
Wakati John akiandika hivyo, Kidoti
Mercy kwenye akaunti yake ya Facebook aliandika: “Chadema nimewapenda
bureeee, mwaaaaa kwa kumpa nafasi Lowassa, sasa kauli mbiu chagua
Lowassa kwa maendeleo ya nchi.”
Aidha, Amir Amir aliandika kwenye
Facebook yake: “Chadema waliomnadi Lowassa kama fisadi papa leo anakuwa
mgombea wao, aibu yao.”
Mbali na mijadala hiyo kwenye mitandao
ya kijamii, gumzo juu ya mwanasiasa huyo lilitawala kwenye mitaa
mbalimbali jijini Dar kwa baadhi ya watu kusema kuwa kuhamia kwake Ukawa
kajimaliza kisiasa huku wengine wakisema anaweza kuingia ikulu kwa
sababu ana mtaji wa watu
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.