Staa wa Bongo fleva, Emmanuel Elibsriki, ‘Nay wa Mitego’.
NI shidaah!
Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai Lowassa
(pichani) kukaribishwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, mastaa mbalimbali Bongo wameamua na wengine
kushawishiwa kumfuata wakiamini katika uwezo wake kiuongozi,
Chanzo makini kililieleza gazeti hili
kwamba mastaa wote waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa wakati akiwania
kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama
hicho katika nafasi ya urais na baadaye jina lake kukatwa kabla ya
kufikishwa Kamati Kuu (CC), wameamua kuhamia Ukawa kumfuata mwanasiasa
huyo aliyejiunga huko kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
TUJIUNGE NA CHANZO
“Moto huku Ukawa umewaka. Yale makundi
mawili ya M4C (Movement For Change- Chadema) na 4 U Movement (Kundi la
Marafiki wa Lowassa) sasa yameingia kazini. Mkakati maalum umeandaliwa
kuhakikisha kila mwenye ushawishi katika jamii anafikiwa, wakiwemo
wasanii wa sanaa mbalimbali.
“Wameanza na wasanii waliokuwa nyuma ya
Lowassa kwa sababu wanaamini wana wafuasi wao, ambao watashawishiwa
wawashawishi hao watu wao wawaunge mkono katika kuhakikisha wanaing’oa
CCM madarakani,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu.
WEMA AKARIBISHWA
Chanzo hicho kimeweka wazi kuwa licha ya
wasanii kwa jumla, lakini pia mastaa wenye mvuto mkubwa kwa jamii
watafuatwa wao rasmi, kama ilivyotokea majuzi ambapo mwigizaji Wema
Isaac Sepetu alifuatwa na 4 U Movement (Team Lowassa) kushawishiwa
kujiunga na Team Lowassa.
Wiki iliyopita Wema alitoswa katika kura
za maoni za kuwania Ubunge wa Viti Maalum (UWT-CCM) Mkoa wa Singida kwa
kushika nafasi ya nne, lakini akapokewa kwa kishindo katika mapokezi
yaliyojaza watu jijini Dar.
“Yaani Wema hivi karibuni aliitwa na
watu wa Lowassa kwenye hoteli moja maarufu jijini Dar ambapo ajenda
kubwa ni yeye kuungana na Ukawa kwa vile wanaamini ana mashabiki wengi,”
kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA WEMA
“Ni kweli, juzi nilipigiwa simu na watu
waliojitambulisha kuwa ni Team Lowassa, wakasema wana mazungumzo na
mimi, ilikuwa tukutane Jumanne, lakini nilikuwa na shughuli nyingine
nikashindwa kwenda.
“Tulikubaliana tukutane jana, lakini
sijaelewa hasa ajenda ni nini na kwa maana hiyo siwezi kusema lolote kwa
sasa kama ninaenda Ukawa au la,” alisema muigizaji huyo, alipozungumza
na gazeti hili.
Jacquiline Wolper.
WOLPER ACHOCHEA
Kana kwamba haitoshi, staa mwingine wa
filamu za Kibongo, Jacqueline Walper Massawe ambaye tangu awali alijitoa
muhanga kufa pamoja kisiasa na mbunge huyo wa Monduli, anatajwa kuwa
kinara wa kampeni katika mitandao mbalimbali ya kijamii akiweka wazi
kuwa atamfuata Lowassa popote atakapokwenda kwani ni shabiki wake
mkubwa.
AUNTY LULU RASMI UKAWA
Ahadi kama hiyo ilitolewa pia na
mwanadada Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ aliyetangaza kujiunga rasmi na
Ukawa kwa sababu ya Lowassa.
Kala Jeremiah.
Mastaa wengine ambao wamemfuata Lowassa
Ukawa ni pamoja na Deogratius Shija, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
Kala Jeremiah, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Bahati Bukuku.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.