Kijana Frank Ephraim Simon.
“Natamani
nirudi shuleni hata kama ni darasa la kwanza, kama siyo ugonjwa huu wa
ajabu ningekuwa namaliza kidato cha nne mwaka huu,” ni maneno ya kijana
Frank Ephraim Simon (17), mkazi wa Kijiji cha Viwege, Gongo la Mboto
jijini Dar akizungumza nasi juu ya mateso anayopata.
…Akinyanyuliwa kutoka kwenye kiti.
Kwa mujibu wa dada wa Frank
aliyejitambulisha kwa jina la Adela Ephraim aliyekutwa akimhudumia na
ndugu zake kijijini hapo, tatizo la ndugu yake huyo lilianza mwaka 2008
akiwa mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Toangoma,
kabla ya kuhamia Viwege.
Akiwa ameketi.
“Alianza kwa kuishiwa nguvu mwili mzima
na kuanguka kila alikokwenda. Tatizo hilo lilidumu kwa miezi kadhaa
kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya CCBRT, Dar.
“Hata hivyo, tatizo halikuonekana zaidi ya kushauriwa awe anapelekwa hospitalini hapo kwa ajili ya mazoezi ya viungo.
“Hali yake ilizidi kuwa mbaya kila
kulipokucha, akawa anaanguka mara kwa mara, ikabidi asiendelee na masomo
kwa muda ili atibiwe gonjwa hilo la ajabu.
“Kuna kipindi alikuwa kama amepona, akawa haanguki tena lakini baadaye hali ilibadilika na kurudi kama awali.
“Kufariki kwa baba yetu mwaka 2011,
kulichangia kudhoofika kwa mdogo wetu, hasa baada ya mama wa kambo
kuziteka mali zote, tukakosa hata nauli ya kumpeleka hospitalini.
“Kama unavyomuona (akimuonesha
mwandishi) hawezi kutembea, kujigeuza, amekuwa ni mtu wa kulala, kila
kitu ni wa kusaidiwa, akishika kitu mikono inatetemeka, akilala sehemu
moja kumgeuza ni shida kwa sababu ni mzito mno kwani kichwa pekee ndiyo
kizima, sehemu zingine za mwili ni kama amepooza.
“Tunaomba
Watanzania, taasisi au kampuni itakayoguswa na tatizo hili watusaidie
ili tuendelee kumtibu ndugu yetu kwani hatujui nini hatima yake,”
alisema dada huyo.
Kwa upande wake denti huyo alisema:
“Watanzania, ninaomba msaada wenu, Rais Jakaya Kikwete na viongozi
mnaosoma Gazeti la Amani, ninaomba msaada wenu.
Kwa yeyote aliyeguswa kumsaidia kijana
Frank ili akapatiwe matibabu kama mwanzoni, awasiliane na dada yake
kupitia simu ya mkononi namba 0659406588.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.