Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

BAADA YA CCM KUZIDISHA MUDA WA KAMPENI, POLISI WATOA TAMKO...


Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema kuwa litatoa tamko la jeshi hilo juu ya Chama cha Mapinduzi kuzidisha muda wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za chama hicho wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa wadau wa uchaguzi jana jijini Dar es salaam Kamishna wa Mafunzo na Operasheni wa Jeshi la Polisi CP Paul Chagonja amesema kuwa wanashughulikia suala hilo na muda ukifika watatoa tamko.

Ameongeza kuwa ili uchaguzi uwe wa Amani ni lazima watu wote watimize wajibu wao.

Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwakilishwa na Jaji Mstaafu John Mkwawa alivitaka vyama vya siasa kuzingatia maadili ya uchaguzi waliosaini ili kulinda amani na kuepusha migogoro na uvunjifu wa Amani.

Kwa upande wa mwakilishi toka chama cha ADC Mwanaisha Yemba alivitaka vyama vyenye vikundi vya ulinzi kuwapa sare na alama maalum walinzi wao ili watambuliwe na kila mtu ili wakifanya vujo iwe rahisi kutambulika.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top