Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

NYUMBA YA BATULI YAUNGUA MOTO... PICHA ZIKO HAPA...

BATULI
Staa mwenye mvuto mkubwa Bongo Movies, Yobunesh Yusuph ‘Batuli’

POLE sana! Staa mwenye mvuto mkubwa Bongo Movies, Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amepata pigo kufuatia nyumba anayoishi Mbezi Beach jijini Dar kuungua moto na kuteketeza vitu vyote ndani, Risasi Jumatano lina mkasa wote.
Akizungumza na paparazi wetu juzi huku akilia kwa uchungu, Batuli alisema tukio hilo lilitokea jioni ya Jumamosi iliyopita yeye akiwa saluni kwa ajili ya kwenda kwenye Fainali za Tanzania Movie Talents (TMT) zilizofanyika usiku huo.
Alisema alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kurejea nyumbani kwake na kukuta nyumba hiyo imeungua na vitu vyote vimeteketea.
Vitu vilivyoteketea ni nguo zote za familia, vyombo, viatu, sofa, stuli, redio, tivii, deki, feni. Kifupi, Batuli alisema hakuna kilichotoka salama.

nyumbaAkiendelea kuzungumzia tukio hilo, Batuli alisema kuwa alipoondoka nyumbani hapo kwenda saluni aliwaacha wasichana wawili wa kazi sanjari na mtoto wake.
Alisema: “Wao walipoanza kuona moshi mwingi walikwenda kugonga milango ya majirani lakini hawakupata msaada wa haraka mpaka moto huo uliotokea chumbani ukaenda jikoni ambako kulikuwa na jiko la gesi na kusababisha mlipuko mkubwa.
“Kwa kweli hakuna kitu ambacho kimetoka ndani. Kuanzia nguo na kila kitu hakuna kilichoweza kuokolewa zaidi ya wadada wangu wa kazi na mtoto wangu. Yaani siwezi hata kuzungumza, niko katika kipindi kigumu sana na hapa nahitajika maombi ili niweze kuwa katika hali ya kawaida.”
Msanii huyo alisema kuwa kwa sasa yeye na familia yake wamepata makazi ya muda (hakutaka kuyataja) akimshukuru staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu kwamba alimpa msaada mkubwa.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top