
Wiki hii ni wiki ya mechi za kimataifa kwa upande wa bara la Ulaya wao timu zao za taifa zitakuwa na mechi za kuwania kufuzu kucheza michuano ya Euro2016, ila kwa upande waAfrika timu za taifa zitacheza michezo ya kuwania kufuzu katika michuano ya AFCON 2017.
Cristiano Ronaldo tayari yeye ameshajiunga na timu yake ya taifa ya Ureno na kuanza mazoezi. Timu ya taifa ya Ureno yenyewe itacheza mechi moja ya kirafiki siku ya Septemba 4 dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa kabla ya kusafiri kwenda kucheza mechi na Albania ya kuwania kufuzu Euro 2016.
Alex Sanchez naye amejiunga na timu yake ya taifa ya Chile kujiandaa na mechi za kimataifa za kirafiki ambazo zipo katika kalenda ya FIFA alipiga picha na kuweka katika mtandao wa twitter. Chile wataikaribisha Paraguay siku ya Jumamosi ya Septemba 5.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN



Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.