Leo mpenzi msomaji wangu nitazungumzia mambo ambayo mwanaume anaweza kuyafanya katika kubaini kama mwanamke aliyenaye anafaa kuwa mke au amuweke pembeni atafute mtu mwingine.
Nimeamua kuandika makala haya nikiamini kwamba, si kila unayeingia naye kwenye uhusiano anafaa kuwa mkeo. Wengine ni pasua kichwa kiasi kwamba ukijichanganya na kumuingiza ndani, yatakayokukuta utajuta.
Kimsingi vipo vimitihani vingi unaweza kumpa mpenzi wako lakini leo nataka kukupa mitihani mitano ambayo ukimpa kisha akafaulu, huyo ana kila sifa ya kuwa mkeo.
Kimsingi vipo vimitihani vingi unaweza kumpa mpenzi wako lakini leo nataka kukupa mitihani mitano ambayo ukimpa kisha akafaulu, huyo ana kila sifa ya kuwa mkeo.
Moja; Siku ambayo umepanga aje kwako, hakikisha ndani kwako kuna nguo chafu na vyombo vichafu. Uviweke katika mazingira ambayo ni rahisi yeye akija kuviona. Sasa, kama atakuja na kuvikuta vyombo ni vichafu, nguo zako pia ni chafu halafu yeye akawa hazungumzii suala ya kukufulia na kukuoshea vyombo, huyo muangalie mara mbilimbili.
Mbili; Akija kwako, chukua simu yako kisha piga simu kama vile unaongea na dada ambaye huwa anakuja hapo kwako kukufanyia usafi wa nyumba, jifanye unamwambia kesho asichelewe kufika.
Endapo atasikia mazungumzo yako halafu asiseme ‘baby mwambie tu kesho asije, nitakupigia deki na kukusafishia nyumba’, huyo si ‘wife material’.
Endapo atasikia mazungumzo yako halafu asiseme ‘baby mwambie tu kesho asije, nitakupigia deki na kukusafishia nyumba’, huyo si ‘wife material’.
Tatu; Ukijua kesho atakuja kwako, leo nenda kafanye ‘shopping’ ya vyakula mbalimbali kama vile mchele, unga na mazagazaga mengine. Uhakikishe vinakuwa katika mazingira ambayo ataviona.
Akishafika mpime kwa kumwambia kuwa, chakula kipo ila umeshindwa kumuandalia hivyo muende hotelini mkale au uende ukamnunulie chipsi. Kwa mwanamke ambaye anafaa kuwa mke, hapo atakuambia ‘noo baby, kwa kuwa chakula kipo nitapika tule mpenzi. Lakini ukiona anasapoti suala la nyie kwenda kununua chakula, huyo hafai kuwa mke.
Nne; Siku unamuahidi kumtoa ‘out’, akija kwako unajifanya umekosa amani ghafla na akikuuliza unamwambia kuwa, mama yako anaumwa sana na pesa uliyonayo ndiyo ambayo uliipigia mahesabu ya kwenda kuitumia out.
Akipuuza kuumwa kwa mama yako na kusisitiza muende tu ‘out’ huku akikuambia kuwa ndugu zako wengine watamsaidia, huyo ana walakini.
Akipuuza kuumwa kwa mama yako na kusisitiza muende tu ‘out’ huku akikuambia kuwa ndugu zako wengine watamsaidia, huyo ana walakini.
Tano; Akikutembelea kwako, yeye akiwa sebuleni muwashie TV kisha wewe anza kupika ukimuandalia chakula. Katika mazingira ya kawaida anatakiwa achukue nafasi yake kama mke mtarajiwa lakini akikuacha wewe upike kisha yeye akaendelea kuangalia TV kwa mbwembwe, hapo hamna mke.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo wewe mwanaume unaweza kuyafanya katika kumtesti mpenzi wako kama anafaa kuwa mkeo.Angalizo; kwenye mapenzi usanii ni mwingi mno, wapo ambao wanaweza kujifanyisha sana. Yaani ukampa mitihani hiyo na akafaulu vizuri kabisa lakini ukashangaa ukishamuweka ndani anaanza kukufanyia vitu vya tofauti.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN

Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.