Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

CUF YAKATAA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR... (PICHA KIBAO)...

4Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamadi (Cuf), akisoma taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani) katika mkutano wake na vyombo mbalimbali vya habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar leo.
3Wanahabari wakiendelea kumsikiliza Maalim Seif Sharif Hamadi (Cuf) kwa makini.
5Maalim Seif akiendelea kusoma taarifa yake.
1Mmoja wa wahariri wa chombo kimoja cha habari akiuliza swali kwa Maalim Seif Sharif Hamadi (hayupo pichani) katika mkutano wake na vyombo mbalimbali vya habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar.
3Mkutano huo ukiendelea.
6Waandishi wa habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakichukua tukio hilo.
7Hali ilivyokuwa.
(PICHA: DENIS MTIMA/GPL)
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitakubali kurudia uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hakuna hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi wa Zanzbar kurudiwa na kufanya hivyo ni kuhalalisha vitendo vilivyofanywa na Tume ambavyo vimekiuka katiba.
Maalim Seif ameongeza kuwa subira ya Wanzibar izae haki ili kuepusha machafuko na migogoro ambayo inaweza kujitokeza kutokana na Uchaguzi wa Zanzibar kufutwa na mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kinyume na sheria na katiba ya uchaguzi kwa shinikizo la viongozi wachache na kwa maslahi ya chama kimoja.
Aidha Maalim Seif amemtaka aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ZEC, Salimu Jecha kujiuzulu kwa kuwa alitangaza matokeo kinyume kwa madai ya kuwa na mapungufu.
Mbali na hayo ametaja vipengele vingi vya katiba ambavyo vinaainisha ukiukwaji mkubwa wa uchaguzi huo

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top