Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

BI. INGABIRE WA FDU AVILAUMU VYOMBO VYA USALAMA KWA MAUAJI YA ANSELME... RWANDA...

Kiongozi wa chama cha FDU ambacho hakijakubalika nchini Rwanda Bi Ingabire Victoire ametaka vyombo vya usalama nchini humo kufanya uchunguzi na kubaini waliotekeleza mauaji ya Bwana Anselme Mutuyimana afisa wa chama hicho aliyehusika na habari.
Mutuyimana aliuawa katika mazingira ya kutatanisha na maiti yake ilikutwa karibu na msitu mkubwa wa Gishwati uliokaskazini magharibi mwa Rwanda siku ya jumamosi.
Akizungumza na Mwandishi wa BBC,Yves Bucyana ,Bi Ingabire Victoire amesema kifo cha aliyekuwa afisa wa chama chake akihusika na habari Anselme Mutuyimana kiliwashtua wengi kutokana na mazingira na jinsi alivyokufa :
''Ijumaa tuliwasiliana nikamwambia kwamba niko salama na yeye alikuwa anaelekea nyumbani kwake asilia, baadae ndipo habari ya kifo chake ilijulikana. Wananchi waliomuona alipofika katika kituo cha mabasi ya abiria eneo la Mahoko wanasema kwamba alipotoka kwenye basi alichukua bodaboda lakini pia karibu hapo kulikuwa na gari nyekundu ya watu waliomsubiri. wawili walikuwa na mavazi ya raia wa kawaida wengine wakivalia sare za polisi. kulitokea purukushani kidogo baina yao lakini hatimae baada ya kuona kwamba ndani ya gari kuna watu waliovalia sare za polisi akatii amri kwa kuwa walimwambia kwamba wanataka kumhoji wakampeleka kwa gari hiyo hadi tuliposikia kifo chake.''
Anselme Mutuyimana alikuwa na umri wa miaka 30.aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela mwaka 2014 kwa hatia ya kuchochea uasi wa wananchi dhidi ya serikali.Kwa mjibu wa kitengo cha polisi kinachohusika na upelelezi wa makosa ya jinai,maiti yake ilipatikana karibu na msitu mkubwa wa Nyungwe kaskazini magharibi mwa Rwanda.
Kiongozi wa chama cha FDU ambacho hakijakubalika Rwanda Bi Ingabire amelaumu vyombo vya usalama akisema kamwe havijafanya upelelezi na kutambua wahusika wa mauaji dhidi ya watu wa upinzani aliosema kua wanaendelea kuuawa nchini Rwanda:
''Tutauliza serikali inakuwaje nchi yenye vyombo vya usalama thabiti ,ni vipi watu wanaweza kuvalia sare za walinda usalama na kufanya kazi ambayo siyo yao.Mwaka 2017 kuna mfuasi wetu aliyeuawa katika mazingira kama haya na sasa mwIngine naye anauawa.Tunahoji katika nchi yenye usalama na ambako vyombo vya usalama vinawajibika utasema je kwamba mtu anauawa kisha waliomuua hawafahamiki?''
Ingabire mwenyewe mwaka 2010 alirejea nchini Rwanda akiwa na nia ya kugombea kiti cha urais ,lakini akahukumiwa kifungo cha miaka 15 kwa hatia ya uhaini kabla ya kuachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kutumikia miaka 6 jela.
Polisi imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya afisa wa chama cha FDU.
Source BBC Swahili

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top