Tani 11 za samaki aina ya Sato zimeteketezwa baada ya kubainika kuwa wana vimelea vya sumu. Samaki hao ambao wanaripotiwa kuingizwa nchini kwa njia za panya kutoka nchini China wana thamani ya dola za Marekani 33,000
Waziri wa mifugo na uvuvi nchini Tanzania, Luhaga Mpina amesema watu walioingiza samaki hao nchini walitumia njia zisizo halali.
Samaki hao walitelekezwa baada ya mamlaka kukamata shehena hiyo, Kama ilivyo ada samaki hao walipitia kwenye vipimo kabla ya kuamuliwa kupigwa mnada, ndipo walipobaini kuwa samaki hao wana kiwango kikubwa cha kemikali ya Zebaki ambacho ni hatari kwa matumizi ya binaadamu.
Aina nyingine ya sumu iliyopatikana kwenye samaki ni viatilifu vya DDT.
Mamlaka zimetahadharisha watu kutofanya biashara kinyume cha taratibu kuepuka kufilisiwa na upoteza mitaji yao,
Sababu ya kukamatwa kwa shehena ya Samaki
Kutokuwepo kwa nyaraka zinazo onyesha kama samaki wameidhinishwa kuingia nchini kutoka kwa mamlaka ya nchi walikotoka
Nyaraka kuonyesha kuwa wamezalishwa au kuvuliwa kwa njia halali huko walikotoka.
Kutoonyesha samaki wamezalishwa na kiwanda kilichoidhinishwa na nchi husika kufanya shughuli za uzalishaji au uvuvi
Kutokuwepo kwa Nyaraka kuonyesha kuwa samaki ni salama ili kulinda afya ya mlaji
Kisha kutoonyesha alama ya kuonyesha jina la muagizaji wa samaki
Wizara imesema samaki hao wangesababisha hatari kubwa kwa walaji, madhara ambayo yangejitokeza siku za usoni kama vile maradhi ya saratani, matatizo katika mfumo wa uzazi na watoto kuzaliwa wakiwa na matatizo ya akili..
Source BBC Swahili
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.