Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.
Kampuni hiyo ya Marekani imesema itasitisha usafiri wa ndege zote 371 zinazohudumu.
Shirika linalosimamia usafiri wa anga Marekani FAA, limesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.
FAA awali lilisisitiza ndege ya Boeing 737 Max 8 ni salama wakati mataifa mengine yakipiga marufuku usafiri wa ndege hizo.
Ajali hiyo siku ya Jumapili mjini Addis Ababa ulisababisha vifo vya watu 157.
Ni ajali ya pili kuwahi kushuhudiwa ya ndege hiyo chapa Max 8 katika miezi mitano baada ya ajali nyingine nchini Indonesia mwaka jana Oktoba iliosababisha vifo vya watu 189.
Shirika la FAA limegundua nini?
FAA lina kundi la maafisa wanaochunguza mkasa huo katika eneo ambalo ajali ya shirika la ndege la Ethiopia ilipotokea likishirikiana na bodi ya kitaifa ya usalama wa safari.
Dan Elwell, kaimu msimamizi katika shirika hilo FAA, amesema Jumatano: " Imebainika wazi kwa pande zote kwamba safari ya ndege ya Ethiopia ilikaribiana na namna ilivyoshuhudiwa kwa ndege iliyoanguka awali ya Lion Air ."
Ameongeza kwamba "ushahidi tuliopata katika eneo, umefanya kuwa na uwezekano mkubwa kwamba hata njia ya ndege ilikaribiana na ile ya Lion Air"
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.