Mahusiano ya mapenzi ni mazuri na matamu sana pale unapokuwa na mtu sahihi katika mahusiano husika, lakini pia yanakuwa mabaya na machungu ya kuumiza sana moyo pale unapokutana na mtu ambaye sio sahihi katika mahusiano husika ambapo upelekea mpaka wengine kufanya maamuzi ambayo sio sahihi na kufikia kupoteza uhai.
Kuna habari ambazo zimekuwa zikizunguuka kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusu Mtu moja aitwaye Daniel Lizy alipokuta message za mbaya katika simu ya mke wake siku 7 tu baada ya ndoa yao kufungwa.
".. najisikia vibaya sana wakati huu, sijui inawezekanaje nikute message mbaya hivi kwenye simu yake wakati ni siku saba tu toka tufunge ndoa,.. na nilichukua simu yake kutaka kucheza game kwa bahati mbaya nikajikuta nimeingia kwenye ukurasa wa Whatsapp ndo nikakutana na haya mambo..." anasema Daniel.
Kulingana na taarifa hizo, kijana anayejulikana kwa jina la Kunle Luv ndo alikuwa anachati na mwanamke huyo Tola ambaye ni mke wa Daniel na alikuwa anamuuliza kwa alikuwa hapokei simu zake wakati Tola akimwambia kuwa alikuwa anafunga ndoa na alikuwa hayuko tayari kuendelea tena na mahusiano yao.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuwa Kunle hakuwa tayari kuachana naye na alikuwa tayari mahusiano yaendelee hata baada ya ndoa hiyom kitu ambacho Tola hayuko tayari kabisa kukifanya hivyo ikapelekea amtangazie dau, yaani aamwambie ni kiasi gani cha pesa alitaka ili tu mahusiano hayo yasitishwe, lakini Kunle alikataa pesa na kutaka mahusiano yaendelea.
Massage zote hizo Daniel alikuwa akizisoma kwenye simu ya mke wake mbichi kabisa ambaye ametoka kufunga naye ndoa wiki moja tu imepita, yaani alihisi moyo wake kupasuka na asijue cha kufanya.
katika siku zote za uchumba wake na mwanamke huyo kumbe Tola alikuwa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa anajivinjari naye wakati huku kwa Daniel akipanga mipango ya ndoa,.. hii kweli ni hatari sana.
kama wewe ni Daniel utafanya maamuzi gani?.. Au ni ushauri gani ambao unaweza kumpa Daniel kama unapewa na fasi ya kumshauri?..
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.