
Habari: na Daniel Michombero MO Design DRC
Kama ilivyo ada kwa watu wengi kusherekea siku zao za kuzaliwa pale inapotimia tarehe hiyo, ndivyo ilivyotokea na kwa Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange, lakini ajabu sherehe hizo za kuzaliwa Rais Kabila zilikuwa kama kituko pale washerekeaji walipoonekana kuwa ni watoto wa shele za msingi tu na baadhi ya wanachama wa chama. chake cha PPRD katika Jimbo la Kasai. MO Design limeipata.
Maandamano hayo yaliyoongozwa na wanafunzi wa shule za msingi, askari polisi wa kike, wanajeshi wa kike na baadhi ya watumishi wa serikali, ni wale tu waliokubali kuorodheshwa kwa lengo hilo la kusherekea siku hiyo ya Tarehe 5 juni. ambayo ni siku ya kuzaliwa Rais Kabila huku wote wakivishwa mavazi ya Mama wa kicongomani.

Maandamano haya ya sherehe hizi yaliyofanyika katika barabara za Mji wa Kananga Jimbo la Kasai ya kati, yaliweka hazarani mgawanyiko wa vyama vinavyomuunga mkono Joseph Kabila na vile visivyomuunga mkono kwani vyama vingi havikuweza kuigia katika maandamano hayo ya Shrehe za kuzaliwa Kabila. vyama hivto ni pamoja na UCP, PANU, PAR na vingine vingi ikiwemo na mashirika karibia yote ya Kiraia, yaligoma kusherekea siku hiyo muhimu kwa Rais wao.

Jumbe mbalimbali ziliandikwa katika mabango ya waandamanaji hao ambao wengi walikuwa wanawake, baadhi ya jumbe hizo ni kama zilivyosema: "Le PPRD soutient le dialogue inclusif" Ikimaanisha "PPRD inaunga mkono Mazungumzo" megine yaliandikwa " Bon Anniversaire Rais Que Dieu te Protege d' avance" ikimaanisha "Siku njema ya Kuzaliwa Rais, Mungu akulinde"
wengine waliandika kuwa wanaunga mkono mahakama kuu ya katiba katika lengo lake dhidi ya Uchaguzi.
Lakini katika hali isiotarajiwa, hata wale wanachama ambao ni nguzo kwa Rais Kabila, hawakuonekana katika maandamano hayo, kama vile Mwamba Kantu Kanjila na wengine.
habari zinazidi kunyetisha kuwa hata katika majimbo mengine mengi nchini humo, hakuna kitu chochote kilichofanyika katika kusherekea siku hiyo, mfano ni jimbo la Kivu Kaskazini na kwingineko.
Mpaka sasa kinachosubiriwa nchini humo ni uchaguzi ambao watu wengi wako gizani kwamba Rais kabila hayuko tayari kuachia madaraka na kuheshimu katiba ya nchi.
Na Daniel Mchombero MO Design DRC
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.