Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

UNENE NOMAAA..!ABIRIA WA NDEGE WATAKIWA KUPIMA UZITO KABLA YA KUSAFIRI

Raia wawili wa American Samoa wamelalamikia kulazimishwa kupima uzani



Image 
Image captionShirika la Ndege limewataka abiria wake kupima uzani

Shirika moja la ndege Marekani limelalamikiwa na wateja wake kwa kuwalazimisha kupima uzani kabla ya kuingia ndani ya ndege zao. Malalamiko hayo yametolewa na wafanyibiashara wawili kutoka Kisiwa cha AMERIKAN SAMOA
Wawili hao wameiambia Mamlaka ya uchukuzi nchini Marekani kwamba walilazimishwa kupima uzito wao wakati wakianza safari yao kutoka mji wa Honolulu. Kituo cha Radio nchini NEW ZEALAND kimesema raia hao walikerwa sana waliponyimwa haki ya kuchagua viti vyao kwenye ndege kutokana na uzito wao. Walikua wakitoka Kisiwani HAWAII kuelekea mji wa PAGO PAGO.
Masharti ya abiria kupima uzani yamewekewa raia wa Kisiwa cha America Samoa, baada ya Kisiwa hicho kutajwa kuongoza kuwa na watu wanene kupindukia duniani.
Raia wa kisiwa hicho kilichoko Bahari ya Pacific wameripotiwa kupenda vyakula vyenye mafuta mengi na hawafuati lishe bora. Mtu mmoja kati ya watu watatu anaugua kisukari katika Kisiwa cha AMERIKAN SAMOA. Kwa sasa mamlaka ya uchukuzi Marekani imesema inachunguza lalama za wafanyibiashara hao.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top