Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

WALIMU WALIOMPIGA KINYAMA MWANAFUNZI MBEYA WASAKWA

Waziri wa mambo ya ndani Tanzania Mwigulu Nchemba na Rais John Magufuli awali


Image , TANZANIA
Image caption


Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania MWIGULU NCHEMBA amewaagiza maafisa wa serikali kuwasaka walimu watatu wa mafunzo ambao wanadaiwa kumpiga mwanafunzi shuleni.
Video ambayo inadai kuonyesha tukio la mwanafunzi huyo akipigwa imesambaa sana mtandaoni TANZANIAna KENYA.
Kupitia taarifa, BW,NCHEMBA, amesema uchunguzi wa awali unaonesha tukio hilo lilitokea katika shule ya upili ya MBEYA tarehe 28 Septemba.
Walimu hao walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo.
Anasema mwalimu mmoja alikuwa amewapa wanafunzi zoezi la Kingereza lakini baadhi ya wanafunzi wakasusia kulifanya na ndipo mwalimu mmoja "alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo."
"Ndio (hapo) walimu wakamchukua na kumpeleka staff room (chumba cha walimu) na kuanza kumpiga vile," amesema BW.NCHEMBA.
Tangu kutokea kwa kisa hicho, inaarifiwa mwanafunzi huyo hajaonekana shuleni tena.



Mwanafunzi apigwaImage 
Image caption


Walimu wote wanaodaiwa kuhusika katika kumpiga mwanafunzi huyo hawapo shuleni MBEYA kwani wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao.
"Polisi wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali," amesema BW,NCHEMBA.
"Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo."

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top