Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ZARI AMFUNGUKIA DIAMOND PLATNUMZ LIVE BILA CHENGA

ZALI & DIAMOND

ZARI The Boss Lady; ni baby mama wa supastaa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz anayeiwakilisha vyema Tanzania ambaye ametema nyongo kwa kumchamba jamaa huyo laivu bila chenga.

Ikumbukwe kwamba, Zari; raia wa Uganda anayeishi nchini Afrika Kusini amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi ambao ni Tiffah Dangote na Prince Nillan.

 

Katika sehemu ya pili ya shoo yao ya Young, Famous and African inayoendelea kwenye jukwaa la Netflix katika Mtandao wa YouTube, Zari anapiga stori na mwigizaji Khanyi Mbau wa Afrika Kusini ambapo anamueleza kwamba aliona ni bora alee watoto wake mwenyewe kuliko kuwa na kinyongo na Diamond ambaye alimsaliti mara nyingi mno.

 

Mwishoni mwa sehemu hiyo ya pili ya shoo hiyo ndipo hapo Zari akawa uso kwa uso na Diamond ambapo anamchamba laivu akifunguka yote mazito ambayo hajawahi kufunguka.

 

Zari anamwambia Diamond kuwa aliwahi kuwaza kuwa na familia yake; kwa maana awe na Zari kama mke hapa na watoto wake hapa?

Hapo Diamond hakuwa na majibu na kumfanya Zari kuendelea kumpa somo kwamba alimkatia tamaa na kumfanya jamaa huyo atulie tuli!

 

Zari anamwambia Diamond: “Unaona ulivyojishusha kama hapa, hukuwahi kujishusha wakati ule tukiwa pamoja, ulikuwa unapanda juu sana, ulijiona staa mkubwa, lakini nadhani leo umeelewa ni hasara kiasi gani umesababisha.”
Zari anaendelea; “Nilikuwa na uwezo wa kupigwa risasi kwa sababu yako kwa jinsi ambavyo nilikuwa ninakupenda.
“Mimi na watoto tulikuwa tunashambuliwa Baba Tee (Diamond), tulikuwa tumechoka, hukutulinda, hukufanya chochote.”

 

Wakati wote huo Zari akiwa anafoka kwa hisia kali na kulengwalengwa na machozi, Diamond alikuwa anatazama pembeni na kujigeuza asijue nini cha kujibu kwa namna alivyomuumiza kutokana na usaliti aliomfanyia kiasi cha kuzaa nje ya uhusiano wake ambapo alizaa na Hamisa Mobeto.

 

Itoshe kusema kuwa, kwenye shoo hii, hasa sehemu hii ya pili, Zari amemtolea uvivu Diamond na kutoa kile kilichoukamata moyo wake juu ya mzazi mwenzake huyo, jambo ambalo hakupata kulifanya.
Kwa kufanya hivyo, wengi wanaamini kuwa, Zari atakuwa ametoa kitu kikubwa na sasa roho yake itakuwa kwatu kabisa.

SIMULIZI ZA CHUMBANI - MAM'DOGO LISA EPISODE 4

 
 KATIKA SIMULIZI ZA CHUMBANI LEO TUNAKULETEA KISA CHA MAM'DOGO LISA SEHEMU YA 4,.. Endelea kupata burudani hii ya kusisimu, kumbuka hii inakujia kwa sauti badala ya maandishi

SIMULIZI ZA CHUMBANI - KISA CHA MAM'DOGO LISA EPISODE 3 (SAUTI)

HIHI HAPA SEHEMU YA 3 YA KISA CHA MAM'DOGO LISA KATIKA SIMULIZI ZA CHUMBANI, Usikose kupata uhondo wa kisa hiki kinachokujia katika sauti na kuboresha zaidi ili uweze kuburudika zaidi,.. na sasa kitakwenda mpaka mwisho...

IDRIS ELBA KUIGIZA KAMA JAMES BOND KATIKA 007 MPYA


PRODUCERS  wa filamu za 007 James Bond, Barbara Broccoli na Michael G. Wilson wamethibitisha kuwa Jina la Idris Elba ni miongoni mwa majina yaliyotajwa wakati wanaongea kuhusu mwigizaji wa kuigiza kama James Bond baada ya Daniel Craig kumaliza filamu yake ya mwisho ‘No Time to Die’.

 

Hii ni filamu ya 25 ya James Bond. Majina mengine yaliyotajwa kwenye mazungumzo hayo ni Tom Hardy, Henry Cavill na Regé-Jean Page.

 

Oktoba 2021 Elba alisema hatachukua kazi hio ila kuna wakati alifikiria na alikuwa na shauku ya kuigiza kama 007 James Bond. Elba ameshaonyesha uwezo mkubwa wa kuigiza kupitia show kubwa za tv kama Luther, The Wire na filamu ya The Suicide Squad.

MO Designtz


 

NAY AWACHANA LIVE WASANI WAPENDA MAGARI NA LEBO


KUTOKA kwenye insta story ya Rapa Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameandika; “Yani kujifanyaga mnawapa magari ooh label kubwa alau mkishindwana mna wapokonya magari yenyewe tena wasanii kwa wasanii.

 

“Ndio mjifunze wasanii wapenda magari ya bure wakati mna vipaji na wakati mkikomaa mnaweza kununua ya kwenu kwa hela zenu coz muziki huu una hela huu ndio maana wao wanaweza hata kuwadanganya na hayo magari na kuwadhalilisha kwa kuwapokonya... hunijui limeboa soon napiga tour najinunulia ligari langu lingine likubwa,” ameandika Nay.

Unahisi, Nay amelenga wasanii gani au label gani ambao wanawapa magari wasanii wao na kuwanyang’anya?..



SIMULIZI ZA CHUMBANI - KISA CHA MAM'DOGO LISA EP 2 Hii hapa ni sehemu ya pili ya kisaha hiki cha MAM'DOGO LISA inayokujia katika mfumo wa sauti, naamini utaoata burudani murua sana... shuka nayo
HARMONIZE AACHANA NA MPENZI WAKE MZUNGU

Huenda penzi la mwanamuziki na C.E.O.wa KondeGang Harmonize na mpenzi wake mzungu ambaye ni raia wa Australia Bryana likawa limevunjika kulingana na mfululizo wa post zake kupitia insta story yake.

Ikumbukwe kuwa penzi la Harmonize na Briana lilianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana miezi kadhaa tu baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake Kajala.

Mbali na hayo mwanamuziki huyo ametangaza kuachia wimbo wake mpya siku ya kesho unaitwa ‘Mwaka Wangu’

DAVIDO NA WIZKID WAMALIZA BIFU


 WASANII wakubwa Barani Afrika na duniani, Ayodeji Ibrahim Balogun almaarufu kama  ‘Wizkid na David Adedeji Adeleke almaarufu kama ‘Davido’ wamemaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda na sasa hivi wakikutana ni amani kama inavyoonekana kwenye picha.

Hii imetokea jana baada nguli hao wa muziki barani Afrika kukutana club nchini Nigeria na kukumbatiana kwa furaha, jambo ambalo limeleta furaha kwa mashabiki wao pia kuona wakipatana tena na kuwa kitu kimoja.








SIMULIZI ZA CHUMBANI - MAM'DOGO LISA EP 1
 
  Katika SIMULIZI ZA CHUMANI, Tunakuletea KISA CHA MAM'DOGO LISA kkatika mfumo wa sauti ili u enjoy zaidi, wale waliokifuatilia kisa hiki katika maandishi sasa mtakifurahia katika mfumo wa sauti na sasa kitakwenda mpaka mwisho maana tuliishia njiani nikimaanisha sehemu ya 27...

HUU NDIO WIMBO MAALUM MSIBA WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI... NI SIMANZI NA MAJONZI...

 

© Copyright MO Design
Back To Top