.. alikuwa amekoseshwa utamu wa siku hiyo na aliokuwa ameukusudia na kuufikiria kila wakati. akaamua kubadilisha ratiba na kwenda mazoezini lakini kichwani kwake akiwa tayari amejiwekea mkakati atakaoufanya siku hiyo... SASA ENDELEA NA SEHEMU YA 21...
... Alifanya mazoezi lakini mazoezi yake ya siku hiyo hayakunoga kwani alikuwa na mawazo mengi kichwani. muda wote wa mazoezi yake alikuwa akipanga ni jinsi gani atapata raha siku hiyo kwa mtoto Hasina. siku hiyo hakufanya mazoezi kama kawaida ya siku zote, alifanya kidogo tu kisha akarudi nyumbani. hata Dennis alishangaa kuona Siku hiyo baba'ke anamaliza mazoezi mapema kwani sio kawaida yake, siku zote akienda mazoezini hutumia masaa mawili lakini siku hiyo alitumia nusu saa tu akarudi nyumbani. alipoingia ndani alimkuta Dennis akiendelea kufuatilia taarifa ya habari. akampita bila kuongea neno. lakini Dennis alipogeuka na kumuona akamuuliza
... baba, mbona leo mazoezi umemaliza mapema?..
... ndio... nataka niwahi ofisini kuna kazi nyingi za kufanya..." aliongea huku akielekea chumbani kwake. lakini kabla hajaingia akageuka na kumuuliza Dennis.
"... kwa leo unaratiba gani Dennis?.."
"... leo mimi sina ratiba yoyote, nitashinda hapa..." alijibu Dennis bila ya kumuangalia baba yake. jibu hilo lilimkera sana mzee huyo kwani alitaka kujua ni muda gani pale patakuwa free ili aweze kurudi na kufanya mambo yake. akiwa bado amesimama hapo mlangoni akampachika swali jingine la kizushi.
"... kwa hiyo siku nzima utashinda unaangalia taarifa ya habari..." alihoji mzee Bisu huku akijaribu kuficha hasira zilizokuwa zinamfukuta moyoni kuhusu mwanaye huyo kutaka kumkosesha alichokikusudia siku hiyo.
dennis aligeuka na kumuangalia baba yake ambaye naye alikuwa akimuangalia na huku akisubiria jibu.
"... kwani baba kuna sehemu ulitaka twende wote?.." swali hilo lilikuwa gumu kidogo kwa mzee huyo kwani hakutegemea kama ataulizwa swali hilo, akili yake ikafanya kazi haraka na akapata jawabu.
"... hapana,... naona kuwa hii likizo itakubwetesha sana, kushinda unaangalia tv bila kufanya kitu cha msingi naona kuwa itakupotezea vitu vingi sana..." aliongea kwa kirefu ili kumuweka sawa mwanaye huyo asimuhisie kitu. Dennis alijikuta akiwa mpole kwa jibu la mzee huyo, akagundua kuwa kweli hawezi kukaa siku nzima nyumbani akiangalia tu tv, akaamua kuweka wazi ratiba yake ya siku hiyo.
"... ni kweli baba, ukweli ni kwamba sio kuwa siku nzima ntakaa tu hapa naangalia tv, baada ya chakula cha mchana ntakwenda matembezini, vile vile kuna kitu ntakifuatilia huko kigamboni..."
jibu hilo lilimfurahisha sana mzee Bisu lakini hakupenda kuionesha furaha yake kwani mwanaye angehisi kuna kitu amepanga kukifanya. kabla ya kuingia chumbani akaamua kuuonesha ubaba wake ili kupoteza malengo ya kile ambacho mwanaye huyo angeweza kukihisia.
"... nafikiria nikutafutie sehemu ya tuisheni ili uwe unakwenda kuongeza elimu na sio kukaa tu hapo unaangalia tv..." wala hakuwa na mpango huo ila aliamua kusema hivyo ili kupoteza maboya ya kutokuonesha furaha yake. akazama chumbani kwake ambako alimkuta mke wake ndo kwanza anaamka, akamsalimia na huku akivua nguo zake za michezo kwa ajili ya kujiandaa kwenda kazini.
"... habari za asubuhi..."
"... nzuri... heh,... ina maana umeshamaliza mazoezi?.. kwani saa ngapi saa hizi?.."
"... bado mapema sana ila mimi tu ndo nataka niwahi kuondoka..." aliongea huku akianza kuingia bafuni.
"... basi ngoja nikamuamshe dada aandae chai mapema..." aliongea Bi. Pauline huku akijivutavuta kutoka pale kitandani.
"... hapana, muache apumzike mimi ntakunywa chai cantine..." aliongea na kuzama bafuni ambako haikumchukua mda mrefu sana tofauti na siku zote ambapo akiingia bafuni lazima atumie nusu saa ndio atoke. siku hiyo kila kitu kilikwenda kwa haraka kwani alitaka muda ukimbie ili muda ule alioutaka yeye utimie na afanye kile alichokikusudia. siku hiyo ni dhahiri kuwa alikusudia sana kufanya kitu hicho. haikumchukua muda mrefu kujiandaa, akaaga na kutoka kuelekea ofisini kwake ambako nako kazi zilipigwa fastfasta. lakini pamoja na fastafasta aliyokuwa nayo muda ulikuwa ukitembea kwa mwendo wake wa kawaida kitu ambacho kilionesha kumkera, kwani kila alipokuwa akiitazama saa yake aligundua tu ni dakika tano zimepita toka alipoiangalia tena. akaendelea kuwa mvumilivu hivyohivyo mpaka ikatimia saa saba kamili. akaviweka vitu vyake sawa pale mezani kwake akijiandaa kutoka. lakini baadae akakumbuka kuwa Dennis alimuambia kuwa baada ya chakula cha mchana ndio atatokana kwenda kwenye mizunguuko yake. na muda huo wa saa saba ndio muda wa chakula nyumbani kwake, akaamua kuvuta muda tena. mpaka ikatimia saa nane kamili. akafunga ofisi yake akatoka na kumuaga secretari wake ambaye naye alishangaa kumuona bosi wake siku hiyo akitoka mapema, kwani huwa hana kawaida ya kutoka hata muda wa lanchi yeye huwa anabaki ofisini.
***************
baada ya kupata chakula cha mchana Dennis hakupenda kupoteza muda, alimuaga mama yake kuwa anatoka na atarudi jioni.
"... hata mimi natoka, nataka niende kwenye mambo yangu..." aliongea Bi. Pauline akiwa anamalizia chakula chake.
"... basi tutakutana jioni..." alijibu Dennis huku akitoka. alipotoka haikuchukuwa muda murefu Bi. pauline naye akajiandaa, alipokuwa tayari akamuaga Hasina kuwa aangalie nyumba vizuri kisha naye akatoka.
***************
Mzee Bisu aliliwasha gari lake na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake, akili yake yote ilikuwa inawaza kile alichokuwa anakwenda kukifanya nyumbani, akipiga picha mambo ambayo Hasina alimfanyia, alijikuta mwili ukimsisimka na kutamani gari lipae ili awahi kufika. ni kweli gari lilikuwa linapaa kwani alikuwa akiliendesha kwa mwendo wa kasi ukizingati kuwa mida hiyo foleni za barabarani zilikuwa chache. aliliendesha gari mpaka akatokea mtaani kwake. akiwa ndio anakata kona ya kuingia katika mtaa huo akamuona Mke wake Bi. Paulene na yeye ndio anatoka getini kwake, akafunga breki za ghafla na kulipaki gari pembeni kwa haraka.
NINI KITAENDELEA? USIKOSE SEHEMU YA 22
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.