Kuna Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba huko Ilula Mkoani Iringa hali ni tete. Wananchi wenye hasira wamevamia kituo cha polisi na kukichoma moto pamoja na magari.
Habari zinasema kuwa chanzo cha sakata hilo ni askari mmoja wa jeshi la polisi kumpiga mwananchi na kusababisha kifo chake. Inaelezwa kuwa Tafrani ni kubwa sana huko na wananchi wanakimbilia milimbani kusalimisha uhai wao, kwani kikosi cha FFU kimeagiza askari wengine kutoka Iringa mjini kwa ajili ya kudhibiti hali hiyo.
Taarifa zinadai kuwa polisi waliokuwa kwenye operesheni ya kukamata watu wanaouza pombe na kunywa muda wa kazi, lakini katika operesheni hiyo, mama mmoja alikurupuka na kukimbia, lakini akawa amekurupushwa na askari aliye chota mtama na mama huyo akaanguka na kufariki hpapohapo. Taarifa zinasema kuwa Mkuu wa kituo alipoulizwa na wananchi kuhusiana na kifao cha mama huyo, akawajibu wananchi kuwa nendeni mkazike,
kauli ambayo iliwachukiza wanachi na kuamua kumshushia kipigona vurugu kuanza rasmi.
inadaiwa kuwa traffic walikimbilia kwenye basi la abiria la Princes Muro, lakini basi hilo likashambuliwa kwa mawe na mwisho kuchomwa moto, mabasi mengine kama 40 wamegoma safari.
endelea kufuatilia modesigntz beste wanguna mimi ntaendelea kukusogezea kila story inayonifikia.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU ILI NAWA UJIUNGE NA KUWA MWANACHAMA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE POPOTE ULIPO
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN


Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.