Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MTU SHUJAA AMUUA MAMBA MKUBWA ALIYEMLA MKEWE MWENYE UJAUZITO WA MIEZI 8


Mwanamke mmoja Demeteriya Nyabwire nchini Uganda, aliliwa na mamba akiwa  anakwenda kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.
mwanamke huyo ambaye alikua na ujauzito wa miezi minane, aliamka asubuhi siku ya Jumapili na kwenda kutafuta kuni katika mwambao wa ziwa Kyoga ambapo alivamiwa na mamba na kuliwa mzimamzima.
Story haikuishia hapo kwani mumewe Mubarak Batambuze (56) wa Kijiji cha Kibuye, alipata habari hizo na kujiapiza lazima atalipiza kisasi cha mke wake.
alichokifanya alikwenda kwa mfuavyuma akaomba kutengenezewa mkuki na baada ya hapo akaingia mawindoni. alikwenda maeneo ambayo mke wake alipita akiwa anatafuta kuni na kweli alimkuta mamba huyo akiwa kapumzika baada ya msosi huo na kupambana naye mpaka akamuua.
Habari zinasema kwamba Batambuze amekuwa Shujaa wa Kijiji maana wanakijiji walifurahishwa na ushujaa aliouonesha kwani mamba huyo anasadikika kuwala wanawake wengine sita na watoto waliokuwa wakienda kuchota maji.
Afisa mmoja wa wanyamapori (UWA) amesema kuwa Mamba huyo alikuwa mkubwa sana kwani ana urefu wa futi 25 na Uzito wa zaidi ya Kilogram 1,000 kg

Endelea kufuatilia modesigntz Beste wangu na mimi ntaendelea kukuletea kila story inayonifikia.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU ILI NAWE UWE MWANACHAMA NA HABARI ZEU ZIWE ZIKIKUFIKIA MOJA KWA MOJA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top