Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

NAY ADATA, SASA KUPIMA DNA KWA AJILI YA MWANAYE... SOMA HAPA



Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’.

KUFUATIA sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo amesema yupo tayari hata kwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu.
Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay, bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji.
Akizungumzia swala hilo, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.

Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ na Siwema Edson wakiwa na mtoto wao.

“Ujue najiuliza sana maana ya kuongelea hili jambo mitandaoni, kusema Curtis siyo mwanangu, kiukweli ninamuacha aongee anavyotaka lakini nasisitiza kuwa ninampenda sana mwanangu,” alisema Nay wa Mitego.
“Niko tayari kupigana hadi tone la mwisho ili mwanangu aweze kuishi kwa amani na upendo na wala sioni tena kama kuna haja ya kuyapa nafasi maneno ya mtandaoni kwa sababu naamini Curtis ni mwanangu na nipo tayari hata kupima DNA nikibaini siyo wangu  nitajua la kufanya,” alisema Nay.

Endelea kuperuz modesigntz Beste wangu na mimi ntaendelea kukushushia ma stori yanayonifikia

USISAHAU PIA KU LIKE PAGE YETU ILI NA WEWE UWE MWANAFAMILIA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top