Msanii wa muziki wa Bongo Flava Mr Blue ana sababu kubwa sana ya kufurahia siku hii ya leo, muda mchache uliopita Mr Blue ameshare na sisi furaha yake kubwa ya kumkaribisha mtoto wake wa pili duniani… kupitia mtandao wa Instagram yake Mr Blue amepost picha ya mtoto wake na ujumbe wa shukrani unaosema..
>>>“Alhamdulilahi Mungu ni mwema sana sana… hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuabudu kumtukuza na kumshukuru, namshukuru sana Mungu wangu na nashukuru pia mke wangu @wahyda_bysers_heart kwa kuniletea zawadi nyingine nzuri… nimepata mtoto mwingine wa kike ndugu zangu anaitwa #khairriyaaa… ahsante Mungu kwa kunipa baba na mama wa kunilea tena uzeeni…”<<< @mrbluebyser1988.
Hongera sana Mr Blue kwa kupata mtoto wa kike!
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN

Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.