Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

OMMY NA CHAKA KUPAMBANA VIKALI NA AKINA DIAMOND NA ALLY KIBA...VURUGU ZIMEANZA (ONA VIDEO HAPA)

Mwanamziki Chipukizi wa Muziki wa Kizazi Kipya Omary Bakari a.k.a Ommy Janja, ameachia Ngoma yake Mpya "CHANGAMOTO" akiwa Amemshirikisha Mwanamziki mwenzie ambaye naye ni Chipukizi ajulikanaye kwa jina la Longino John a.k.a Chaka Mlingula. Ngoma hiyo imeachiwa hivi karibuni kupitia vituo vyote vya TV na vile vya Radio.
Akiongea na MO Design Ommy Janja Amesema anaamini kuwa ngoma hii ndio itakayomuweka pazuri zaidi katika ulimwengu wa mziki, ukiachana na ngoma yake ya kwanza kabisa iliyokuwa ikijulikana kwa jina la "MANENO MANENO SOO"
Ommy janja ameiambia MO Design kuwa sasa amekuja kupambana vikali na wakongwe wake kama akina Diamond na Ally kiba ambao ndio wameshikili game la mziki wa bongo flava kwa sasa, kwani anaamini kupitia kipaji chake naye atafikia hapo walipo.

CHEKI VIDEO
 
Lakini pia Chaka ambaye ni mshirika mwenzie Ommy, aliiambia MO Design kuwa, hakuna kukata tamaa na mapambano yanaendelea, akajaribu kutoa methali ya kwamba "WAO WAWEZE WANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI?
Hapa alikuwa akimaanisha kuwa hao wanaoshikilia Gamu kwa sasa wana nini? kwani hata wao uwezo wanao na wataweza tu, Chaka Mlingula anatamba kwa sasa na kibao chake kiitwacho "SIDHANI KAMA NTAPENDA" Ambayo ipikwenye mitandao yote katika mfumo wa Audio na Video.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top