
STRAIKA wa Paris Saint-Germain (PSG) Zlatan Ibrahimovic amethibitisha kuwa anatarajia kuhama kikosini hapo kwenye dirisha la usajirli, msimu wa majira ya joto (Mara tu baada ya kumaliza msimu huu).
Ibrahimovic amekuwa akiwaniwa na vilabu vya Manchester United na Arsenal, hii itakuwa ni mafanikio ya kuimarisha kikosi kwenye kilabu itakayofanikiwa kumsajili msimu ujao.
Straika huyo ambaye ni raia wa Sweden, ana umri wa miaka 34 bado haijafahamika bayana kuwa nani atamsajili japo hivi karibuni, Man United ndiyo imeonekana kupewa nafasi kubwa zaidi ya kuidaka saini yake.
‘Sitakuwa PSG msimu ujao,’ alikaririwa na the Guardian.
Ibrahimovic amefunga magoli 377 na kufanikiwa kunyakuwa mataji makubwa 26.
‘Nimebakisha mwezi mmoja na nusu ili kumaliza mkataba wangu. Nitafurahi nikiwa hapa. Kitakachotokea mwakani sijui lakini nachoweza kusema sitokuwa tena hapa.’
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.