Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MR. RAVI WA STEPS INTERTAINMENT NA SPLASH KUWAPA SHAVU WASANI CHIPUKIZI WA FILAMU



Watazania wengi wanaitazama kwa jicho tofauti Tasnia ya Filam Tanzania kwani inaonekana kushuka sana tofauti na ilivyokuwa zamani., lakini pia wengi husema kuwa Kifo cha marehemu Steven kanumba ndio chanzo cha kushuka kwa Tasnia hiyo wakati wengine wakisema hakuna jipya.

Mo designtz tulitembea kampuni kubwa za Usambazaji wa filam za STEPS INTERTAINMENT pamoja na SPLASH tukakutana na Managing Director wa makapuni hayo Mr. Ravi  Solanki.
yeye alikuwa na haya yakusema.
" mimi naungana na hao wanaosema hakuna jipya kwani wasanii wengi wamebweteka kwa sababu ya majina makubwa so wanatunga story zisizo na mvuto kwa kutegemea watu watapenda tu kwa vile filam ina msanii Fulani.. ni kweli watu wana taka kumuona msanii Fulani lakini pia wanataka kuona huyo msanii amefanya kitu kizuri, sasa wakiona msanii wanayemtaka anafanya kitu sio kizuri ndio hapo wanaposema kuwa hakuna jipya... aliongea Mr Ravi
Lakini pia  alisema kuwa yeye kama yeye analengo la kuleta mabadiliko kwani anaamini kuwa kuna watu wengine ambao hawajawahi kuonekana lakini wanawezakuwa na uwezo mkubwa na kufanya vitu vikubwa vya kuifuraisha na kuishangaza jamii.
"... una jua kaka mimi nataka kuleta mabadiliko katika Tasnia hii kwani naamini kuwa mitaani huko kuna wasanii wengi wenye uwezo na ambao wanaweza kufanya vitu vikubwa sana na jamii itashangaa... kwa hiyo kaka hili ninalikuambia ni ukweli kabisa STEPS sasa hivi tutapokea Filam za wasanii wote bila kujali huyu ni msanii mdogo au mkubwa, tutachoangalia ni kuwa filamu inaubora kuanzia picha mpaka story tukijiridhisha filamu tutaichukuwa na tutaisambaza..." alisema Ravi
Mr. Ravi ametoa Rai kwa wasanii wajitahidi kufanya filam nzuri tu kwani yeye hatobagua Super Star wala Underground kwani lengo ni kupata wasanii wengine wazuri ili kujaribu kuipandisha zaidi Tasnia hii ya filam.
ilizoeleka kuwa filam zilizokuwa zikissambazwa na Kampuni ya STEPS na SPLASH ni zile za wasanii wenye majina tu, lakini Mr. Ravi amefunguka kuwa sasa ni Ruksa hata kwa wasanii wa dogo kupata na fasi ya kusambaziwa filam zao ila tu ziwe na ubora unaotakiwa.
Mo design sisi tunasema hongera sana Mr Ravi kwa maamuzi hayo mazuri yasiyo na ubaguzi kwani mitaani kuna wasanii wengi na wenye vipaji maamuzi yako yatawasaidia pia. na hii inaonyesha ni jinsi gani unaitekeleza Kauli ya Rais wetu John pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU...

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top